Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (2024)

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wengi hula kuku. Hata hivyo, je, kuna vitu vyenye madhara na kemikali kwenye kuku wanakula? unaelewa jinsi ya kujua hilo?

Kulingana na data iliyotolewa na Idara Kuu ya Uvuvi na Ufugaji Wanyama mnamo 2019, Tamil Nadu ndio mzalishaji mkubwa wa kuku wa nyama nchini India.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tume ya Kudhibiti Wafugaji wa Kuku (PFRC), thamani ya sekta ya kuku katika uchumi wa nchi ni Rs.2,04,900 crore..

Kulingana na kampuni ya Ujerumani ya kuchakata data 'Statista', tani 4,407.24 za nyama ya kuku zilizalishwa na kusafirishwa nchini India mnamo 2023.

Hata hivyo, uvumi mwingi umekuwa ukizunguka kuhusu kuku wa kizungu kwa miaka mingi. Kuna uvumi kwamba sindano na dawa zinazotolewa kwa kuku wa nyama husababisha matatizo mengi ya afya.

Kuku wa kizungu ni yupi hasa? Hukuzwa kwa njia gani? Je, kuna hatari yoyote kwa miili yetu ikiwa tutakula nyama ya kuku hawa? Wacha tuone wataalam wanasema nini juu yake.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuku wa kizungu ni yupi?

Kuku wa kizungu sio kuku wa asili. Kuku hawa hufugwa kwenye mashamba. Hukua kwa muda mfupi sana. Mpango huu ulianzishwa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1930 katika nchi nyingi kama Marekani.

Mwishoni mwa miaka ya 1960, kuku wa nyama walienea ulimwenguni kote. Uzalishaji wa kuku hao uliongezeka kutokana na uhaba wa nyama ya kuku.

Kufika kwa kuku hawa kunaweza kusemwa kuwa muhimu sana. Nyama hii ya kuku ni muhimu hasa kwa nchi nyingi ambako kuna uhaba wa protini.

Kipindi cha kukua, gharama ya chini na protini ya juu ni sababu kuu za ongezeko la mahitaji ya nyama hii.

Muthuramalingam, ambaye ana uzoefu wa muda mrefu katika usimamizi wa ufugaji wa kuku, alisema kuwa ufugaji wa kuku wa nyama ulianza nchini India miaka ya 1970 na ulaji wa nyama uliongezeka sana mnamo 1980-85.

Alisema katika kipindi cha miaka 30 tangu wakati huo, kuku wa nyama wamekuwa wengi kuliko kuku wa asili, na sasa wamekuwa wa kawaida katika kila mkoa.

Kulingana na Tume ya Kudhibiti Wafugaji wa Kuku, wale wanaofugwa kwa muda mrefu kwa mayai hujulikana kama 'layers'. Wale wanaouzwa kwa nyama kwa muda mfupi huitwa 'broilers'.

Kuku wa kizungu ni aina maalum ya kuku wa Cornish. Aina hii ya kuku ina uwezo wa kukua haraka sana. Tangu mwaka 1970, wameanza kufuga kuku wa aina hii kwa ajili ya nyama,” alisema daktari wa watoto na mshauri wa lishe Dk. Arun Kumar.

“Kutokana na mabadiliko ya kisasa katika tasnia hii, kuku wa nyama ambao walikuwa wakikua kwa siku 60, sasa wanakua ndani ya siku 32. Sababu yake ni mabadiliko ya chakula kinachotolewa kwa kuku hawa,” alisema.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, kuna tofauti gani kati ya kuku wa kizungu na kuku wa kienyeji?

Kwa kawaida huchukua miezi sita au zaidi kukuza kuku kienyeji. Lakini, kuku wa nyama hupata uzito wa zaidi ya kilo 2 ndani ya siku 35 hadi siku 45.

Hata hivyo, kuku wa kizungu hawana kinga sawa na kuku wa kienyeji. Kwa hivyo, kuku wa nyama wanahitaji kuchanjwa mara kadhaa.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni sheria gani hutumiwa katika ufugaji wa kuku wa kizungu?

Mtaalamu wa lishe Meenakshi Bajaj anasema kuna miongozo maalum ya ufugaji wa kuku wa nyama.

Tume ya kudhibiti wafugaji wa kuku imetoa mwongozo wa jinsi ya ufugaji wa kuku wa nyama unastahili kufanywa.

Kulingana na miongozo hii, kuku wa kizungu wanapaswa kufugwa kwa muda wa wiki 6 hadi 8.

Miongozo imeamuliwa kuhusu aina gani ya chakula, maji, mazingira ya kulea, chanjo na dawa wanapewa.

Tume ya Kudhibiti Ufugaji wa Kuku inapendekeza ufugaji wa kuku wa kizungu kwa njia yenye afya.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (5)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuku wa kizungu wanadungwa sindano za hom*oni?

Ripoti nyingi zinadai kuwa kuku wa kizungu hudungwa sindano za hom*oni kuwafanya wakue haraka.

Taarifa hizi zinasema kuwa wale wanaokula hupata matatizo yanayohusiana na hom*oni na vifaranga hubalehe mapema. Na, hii ni kweli jinsi gani? Je, ni kweli kuku hawa wanadungwa sindano za hom*oni? Alipoulizwa, Muthuramalingam alisema kuwa jambo kama hilo halitafanyika.

"Kuku hawa wanapokua hushambuliwa na virusi vya aina mbalimbali, sawa na binadamu anavyochanjwa dhidi ya virusi, kuku hawa pia huchanjwa, mbali na hayo hakuna dawa nyingine," alisema.

Naibu Katibu wa Kamati ya Udhibiti wa Wafugaji wa Kuku Sarath alisema kuwa ikiwa hom*oni itawekwa kwa kila kuku, gharama itaongezeka sana.

Hakutakuwa na fursa kama hiyo. Ikiwa kitu kitatokea kwa kuku hawa, antibiotics itatolewa, alisema.

Kuku wa nyama hukua ndani ya siku 42 hadi 45. Hawapewi hom*oni. "Hawa sio kama wanyama wengine wakubwa," alisema.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (6)

Chanzo cha picha, Getty Images

'Hakuna kitu kama hom*oni ya ukuaji'

"Watu wengi wanadhani kuku hawa wanafugwa kwa hom*oni za ukuaji. Lakini hakuna hom*oni kama hiyo. Kwa watoto waliodumaa, hom*oni za ukuaji hutumika kwa watoto ili kuongeza urefu wao. Iwapo zitatumika kwa kuku, wanastahili wapewe nne kila siku kwa siku 40. Hiyo ina maana kwamba gharama itakuwa ya juu.

"Ili kuwakinga kuku hawa dhidi ya maambukizo ya virusi, chanjo 5 hutolewa kwa kila kuku. Wengi wanazichukulia kama sindano za hom*oni," alisema.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (7)

Chanzo cha picha, Getty Images

Je! watoto wadogo huzeeka haraka?

Mshauri Mwandamizi wa Hospitali ya SRM Global Hospital Yashoda Ponnuchami alisema kuwa Utafiti wa Kituo cha Kitaifa cha Tiba cha Marekani uligundua kuwa watoto wanabalehe mapema kuliko kawaida.

Kula kuku aliyepikwa vizuri hupunguza hatari ya matatizo. Lakini, inasemekana kwamba kula biryani katika umbo lake au vinginevyo husababisha kuongezeka uzito na matatizo mengine.

"Tumewachunguza wanawake wanaokuja kwetu. Watu wengi wanasema kuwa nyama ya kuku ni nzuri pamoja na wali. Kutokana na hali hiyo, matatizo kama vile unene wa kupindukia, kukoma hedhi mapema," alisema Jayanthi, daktari mkuu wa lishe kutoka Hospitali ya Misheni ya Meenakshi. Madurai.

Hata hivyo, Dk. Arun Kumar alisema kwamba hii ni hadithi kamili.

"Katika miaka mia moja iliyopita, umri wa balehe umeongezeka kwa watoto wote wasiopenda mboga na wasiokula mboga. Watoto waliokuwa wakibalehe wakiwa na umri wa miaka 17 sasa wanabalehe wakiwa na umri wa miaka 11 na 12. Hii ni kwa sababu miili yao hupata kiwango kinachofaa cha protini inayohitaji Ikiwa watoto hubalehe kabla ya umri wa miaka 8, inaitwa kukoma kwa hedhi mapema Arun Kumar alisema kuwa watoto wanakuwa na afya njema wanapobalehe wakiwa na miaka 12.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (8)

Chanzo cha picha, CHANDRASEKHAR

Kutakuwa na matatizo ya uzazi?

Meenakshi, mtaalamu wa lishe, anasema kwa hakika kuna hatari katika kufuga kuku katika mashamba ya kuku bila kufuata sheria zilizowekwa na Tume ya Kudhibiti Wafugaji wa Kuku.

Aidha, Profesa wa Chuo cha Madaktari cha Serikali cha Chennai Stanley na Mkuu wa Idara ya Matibabu S Chandrasekhar pia alitoa maoni sawa wakati watu wanakula aina hizi za kuku ambao wamepewa kemikali na antibiotics.

“Maelfu ya kuku wanafugwa kwenye viwanda vya kuku kwa kuongeza kemikali kwa kuku hao kwa ajili ya nyama ya ziada.Viua vijasumu vilivyo na nguvu huwekwa kwenye vyakula vyao ili kuzuia virusi vya aina yoyote kuwashambulia.

Kemikali hizi huitwa visumbufu vya endocrine.

Alisema ulaji wa vitu vyenye kemikali hizo unaweza kusababisha matatizo ya kiafya mfano ugumba, uvimbe kwenye tezi dume na kukoma hedhi mapema.

Chandrasekhar alisema kuwa kemikali katika kuku wa nyama sio sababu pekee ya magonjwa haya, lakini hii inaweza pia kuwa sababu.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (9)

Chanzo cha picha, DOCTOR ARUNKUMAR

'Huenda kusikuwe na athari kwa watu'

Dk Arun Kumar alisema licha ya kuenea kwa matumizi ya antibiotics katika ufugaji wa kuku wa kizungu, haziathiri watu moja kwa moja.

“Mara nyingi watu hupewa dawa za kuua viua vijasumu, hivyo vinavyopewa kuku.

Dk. Arun Kumar alisema kuwa kula kuku wa nyama hakuleti hatari kwa wanadamu.

“Kuku wa nyama ni nyeti sana, hutolewa kwa dozi ndogo kuliko inavyotakiwa, dawa hizi za antibiotics hutolewa kwa maelekezo ya daktari wa mifugo. Hakuna nafasi ya kushambulia binadamu Kisayansi hili haliwezekani,” alisema.

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (10)

Chanzo cha picha, MEENAKSHI BAJAJ

Walaji wa biryani wanapaswa kufanya nini?

Uchunguzi wa hivi majuzi umebaini kuwa Biryani ilikuwa chakula nambari 1 kilichoagizwa na makampuni ya utoaji wa chakula nchini India mwaka jana. Wahindi huagiza Biryani kila baada ya sekunde 2.25.

Kuku Biryani ni maarufu sana kati ya Wahindi. Kula kuku kupita kiasi pia ni hatari. Lakini, mtaalamu wa lishe Meenakshi anasema kwamba hatari hizi zinaweza kuepukwa .

"Unaweza kula gramu 100 za kuku mara tatu kwa wiki. Mbali na kukaanga, inaweza kuliwa katika mchuzi au kuchemshwa. Katika kesi ya biryani, kula mara mbili kwa mwezi kwa kiasi. Lakini ni bora kuipikia nyumbani,'' alisema.

Imetafsiriwa na Jason Nyakundi

Je, kuku wa 'kizungu' wanaweza kusababisha matatizo ya kiafya? - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Dan Stracke

Last Updated:

Views: 5845

Rating: 4.2 / 5 (63 voted)

Reviews: 86% of readers found this page helpful

Author information

Name: Dan Stracke

Birthday: 1992-08-25

Address: 2253 Brown Springs, East Alla, OH 38634-0309

Phone: +398735162064

Job: Investor Government Associate

Hobby: Shopping, LARPing, Scrapbooking, Surfing, Slacklining, Dance, Glassblowing

Introduction: My name is Dan Stracke, I am a homely, gleaming, glamorous, inquisitive, homely, gorgeous, light person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.